Baraza la Mawaziri wa Uvuvi la Lake Victoria Fisheries Organization (LVFO) liliagiza Nchi Wanachama kuanza kutoa Leseni kwa kuzingatia aina ya samaki (Species Specific Licensing). Lengo la kuwa na mwongozo ni kuweka utaratibu na mfumo uliooanishwa kwa Nchi tatu zinazomiliki Ziwa Victoria za Kenya, Uganda na Tanzania wa kusajili/kutoa leseni za vyombo vya uvuvi na leseni za Uvuvi na kuhakikisha leseni zinatolewa kwa aina ya samaki.
Vilevile Rasimu ya Mwongozo imeainisha aina ya leseni na vibali vinavyotolewa na Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kwa ajili ya shughuli za uvuvi na masharti (requirements) yanayohitajika ili kukidhi kupatiwa leseni na taratibu (Procedures) za kufuatwa katika mchakato wa kupata Leseni.
Aidha, Rasimu ya Mwongozo imeainisha pia wajibu na majukumu ya wadau mbali mbali ikiwemo Serikali katika kutoa na kusimamia utekelezaji na matumizi ya leseni kwa aina ya samaki (Species Specific).Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inaomba maoni kutoka Wadau wa Sekta ya Uvuvi. Maoni hayo yatumwe katika email stephen.lukanga@nfqclab.go.tz, info@nfqclab.go.tz kabla ya tarehe 22 Juni, 2017 ili kuiwezesha Wizara kuyawasilishwa maoni ya wadau Ziwa Victoria Tanzania kwenye Sekretarieti ya LVFO ifikapo tarehe 26 Juni, 2017 ili yaweze kujumuishwa na kuingizwa katika Rasimu ya mwisho (Final Draft) ya Mwongozo husika na hatimaye kuwasilishwa katika vikao mbalimbali kwa ajili ya kupitishwa.
Jun 14, 2017Round Table meeting to discuss Lake Victoria Nile Perch eco-labelling program to be conducted on 15th June 2017 at ELCT Hotel, Bukoba, Kagera Region. The meeting organized by Supreme Perch Ltd
May 30, 2017Ministry of Livestock and Fisheries, Director of Fisheries Development Division, P.O. Box 2847
40487 DODOMA-TANZANIA
National Fish Quality Control Laboratory (NFQCLAB), Principal Laboratory Officer, Fisheries Area Nyegezi, P.O. Box 1392, MWANZA-TANZANIA
Website: www.nfqclab.go.tz
Simu: +255 784 437 234
Nukushi: -
Barua pepe: Info@nfqclab.go.tz
© 2024 MAABARA YA TAIFA YA UVUVI(NFQCLAB) . Haki zote zimehifadhiwa..